‘Dudu’ ndio ngoma mpya ya mduara kutoka kwa bibiye Shilole ambayo ameitambulisha rasmi juzi katika FNL ya EATV na jamaa aliyeshirikishwa humo ni mkali wa sauti toka kitambo Q-chief
Ngoma hiyo iliyotawaliwa na nyonga za kufa mtu, Shilole katoka kitofauti kidogo na ngoma zake tulizozizoea maana alitupia vazi la shela kama vile anakwenda kufungishwa ndoa kanisani na mchungaji na kumbe swaga tu mziki.
“Mi huwa napotoa kitu huwa sibahatishi na huu ni mwanzo tu wanaosubiri mi nishuke chini nawaambia wajipange sana maana niko kamili gado kivyote kuanzia muziki hadi katika kazi zangu za filamu”. Alisema Shilole
Shilole huko nyuma ngoma yake ya kwanza aliyotoa ilijulikana kwa jina la ‘Nyumba za kupanga’ ambayo pia alimshirikisha Qcheif ilifanya pouwa sana katika gemu, mpango mzima sasa ni kusubiri tuone hiyo ‘dudu’ yake kama itafanya pouwa au mbwembwe tu.
Source: EATV
No comments:
Post a Comment