Showing posts with label STORY. Show all posts
Showing posts with label STORY. Show all posts

Tuesday, January 29, 2013

PICHA MBALI MBALI ZA LULU AKITOKA ENEO LA MAHAKAMA


 Lulu (katikati) akitoka eneo la mahakama baada ya kukamilisha dhamana yake.
Lulu akiwa ndani ya gari baada ya kukamilisha dhamana yake.
Kutoka kushoto ni mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, wakili wa Lulu bwana Kibatala na Dk. Cheni wakijadili jambo wakati wakisubiri dhamana ya Lulu.
Lulu akiingia katika chumba cha msajili wa mahakama ili kukamilisha dhamana yake.
Gari lililombeba Lulu likiondoka mahakamani.
Lulu akishuka katika gari la polisi baada ya kuwasili mahakamani leo.
Lulu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kupata dhamana leo.
 --------------------------------
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumuua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba Aprili 7, 2012 bila kukusudia baada ya kukamilisha taratibu zote za dhamana.

YAWEZEKANA A-Y AKAWA NDIO MSANII PEKEE TAJIRI KWA TANZANIA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na na mwenye tuzo kibao za kimataifa Ambwene Yesaya AY ni kati ya wasanii wanaomiliki pesa nyingi sana na mali kibao lakini hawapendi kujionyesha imefahamika. 

Chanzo makini na cha karibu na msanii huyo kimesema kuwa AY ni msanii anayemiliki pesa nyingi sana na ni kati ya wasanii wenye biashara nyingi sana ndani na nje ya nchi.


Chanzo hicho kiliendelea kupasha kuwa msanii huyo kwa sasa anamiliki mijengo kadhaa ndani ya bongo na maduka lukuki hasa ya nguo na Pub kadhaa japo msanii huyo hapendi kujulikana kama ni vyake kilisema chanzo hicho. 

AY anamiliki vitu vingi sana sema jamaa si mtu wakujionyesha lakini nataka ujue kuwa kuna uwezekano mkubwa jamaa akawa ndio mwanamuziki tajiri Tanzania kilisema chanzo hicho na kuendelea kumwaga za ndani kuwa juzi juzi AY alinunua nyumba hapa dar na yupo mbioni kuivunja na kujenga ghorofa.


Jamaa alizidi kutiririka na kuweka wazi kuwa kwa sasa AY anamiliki mjengo wa ki- star nchini kenya na ana maduka kadhaa katika nchi hiyo. 

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa AY mwenyewe aliwahi kukaririwa akisema kuwa ni kweli ana mpango wa kununua nyumba kenya na kufungua maduka kadhaa hivyo ameona bora kununua nyumba nchini humo kwakuwa ni sehemu ambayo anaenda sana kwa shughuli zake na apate pakufikia na kupanga mambo yake badala ya kukaa hotelini. 

Mwamuziki huyo licha ya kumiliki vyote hivyo bado ana miliki kampuni yake ya Unity Entertainment ambayo inaendelea kukua siku hadi siku na sasa ikiwa na wasanii kama Ommy Dimpoz, Feza Kessy na Stereo kwenye roaster yake.

AY ni msanii wa kwanza Tanzani kwa upande wa muziki mwenye connection kubwa na wasanii marufu wa afrika na ulaya, kwa Afrika alionao karibu kwa ajili ya kazi ni pamoja na P Square, Jay martins, Jose chamilione, Bebe Cool, Prezzo, Aman, Alpha Kwa upande wa marekani ni Romeo,D'Banji,Akon,Master P, Sean King Stone.

HATIMAE LULU KUPATA DHAMANA NA KURUDI URAIANI



Takriban saa moja tangu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilipotangaza kumwachia Lulu kwa dhamana, chanzo chetu mkoani Kagera kilituhabarisha: “Mama Kanumba leo amekuwa mnyonge tofauti na siku zote, aliposikia tu Lulu kaachiwa huru, amejiinamia tu, analia sana.”
Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimpigia simu Mama Kanumba ambaye alipopokea tu, kilio kilisikika.
Wakati analia, Mama Kanumba alisema: “Siumii Lulu kuachiwa, najua ni mapenzi ya Mungu ila naumia sana kwa sababu mwanangu mpenzi nilishamzika.”
 Hata hivyo, mazungumzo hayo yalikoma baada ya Mama Kanumba kushindwa kunyamaza, licha ya mwandishi wetu kutumia muda mwingi kumbembeleza aache kulia.




Saa moja na nusu baadaye, Mama Kanumba akiwa amenyamaza, alimpigia simu mwandishi wetu, akieleza kwamba pale alipo ameshikilia picha ya Kanumba ambayo inamkumbusha machungu aliyokua ameanza kuyasahau.

AKAZUNGUMZA MAZITO
Kuhusu kile kinachomuuma zaidi, Mama Kanumba alisema: “Anayeniumiza ni Mama Lulu, sisi wote ni wazazi lakini hata siku moja hajaja kuniona, kunipa pole, japo najua kilichotokea siyo mapenzi ya Lulu.”

KUNA WAMBEA WALICHAFUA HALI YA HEWA
Mama Kanumba alisema: “Kuna watu wamenipigia simu huko Dar es Salaam kwamba leo kutakuwa na sherehe ya nguvu ya kumpongeza Lulu kupata dhamana.”

Je, hilo lina ukweli? Staa wa Filamu, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ ambaye amekuwa bega kwa bega kuhakikisha Lulu anapata dhamana, alisema: “Hakuna sherehe, hatuwezi kufanya hivyo, jamii haitatuelewa.”

Mama Lulu naye: “Jamani namshukuru Mungu kwa Lulu kupata dhamana, hakuna sherehe. Mazingira ya kesi yalivyo, haitakuwa vizuri kufanya sherehe, haitakuwa ubinadamu.” 

MASHITAKA YA LULU
Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa mcheza filamu maarufu Afrika, Steven Kanumba

Saturday, January 19, 2013

HEMED KUTOKA NA VIDEO MPYA SIKU YA VALENTINE



 Hemed Suleiman baada ya kuachia ngoma yake mpya mwaka jana inayokwenda kwa jina la Going Crazy kutoka B hits, sasa basi anatarajia rasmi kuachia video yake mpya siku ya tarehe 14 Valentine Day.Kaa tayari kwa ujio huu mpya kutoka kwa PHD.

SHAKIRA NA PIQUE NI WAZAZI WATARAJIWA



Ready and waiting: Shakira and Gerard Piqué have posed for a series of intimate shots, showing off her baby bump  

Shakira na mpenzi wake mcheza mpira  Gerard Piqué  wameachia picha kadhaa zinazoonyesha uka uzito wake wakisherehekea ujio wa mtoto wao wakwanza
 akiwa amevaa bikini top na sketi, huku boyfriend akiwa hana shati, picha inaonyesha ukaribu wao wakiwa wanasuburi ujio wa mtoto wao wakwanza wakiume

 Picha hizi ambazo zilipigwa na Jaume Laiguana, zilitupiwa kwenye mtandao mara baada ya wawili hao kuamua kuungana na UNICEF ku host a virtual baby shower.

Not long now: The Colombian singer shows off her amazing pregnant shape in the snaps wearing just a pair of loose-fitting trousers and a bikini top  

Shakira, 35, amefata nyayo za ma staa kama  Demi Moore and Britney Spears,  ambao walishawahi kupiga picha za namna hii wakati wa muda wa mwisho mwisho wa mimba zao.

Pregnant and proud: Shakira and her footballer beau Gerad Pique have posed for this beautiful picture which shows the singer in all her pregnant glory 

Shakira na mchezaji huyu wa FC Barcelona walikutana mwaka 2010, pale alipotokea kwenye music video ya Shakira, (waka waka, this time for Africa) ambao ulikua ndio wimbo wa kombe la dunia.
Beautiful: In the second image, taken as part of the 35-year-old's virtual baby shower alongside UNICEF, Sharkira stands in a flowing almond gown

JOH MAKINI ATOKA KI UTU UZIMA


JOH MAKINI: MASHABIKI WANGU HUU NDIYO UJI WANGU MPYA SOON KUTOKA

Msanii rapper kutoka Arusha, maarufu kama Joh Makini Mwamba wa kaskazini baada ya kufanya vizuri mwaka jana katika tasnia hii ya muziki wa Bongo Fleva,mwaka huu amejipanga vema na siku za hivi karibuni anatarajia kuachia video yake mpya inayokwenda kwa jina la KI-UTU-UZIMA.Kaa tayari kwa uji huo mpya kutoka kwa Joh Makini

Tuesday, January 15, 2013

NIKKI MBISHI NA KINGZILLA KUFANYA MIXTAPE YAO





Wakali wa Hiphop Music BongoNikki Mbishi na Godzilla ambao wote walipata nafasi ya kusikika baada ya mashindano ya Freestyle ambayo yalikua yakiendeshwa na Clouds fm wameamua kufanya Project ya pamoja.

Nikki Mbishi ambaye alitamba na track ya Playboy ambayo alimshirikisha Ben Pol, jana kwenye ukurasa wake wa Facebook ali-announce mpango wa kufanya Project hii na GodzillaNikki aliandika:

"Nikki Mbishi na Godzilla kazini, jiandae kwa Mixtape yetu ya pamoja iitwayo 'KKK'..."

Lately kwenye mtandao wa TwitterGodzilla amekua supporter mkubwa sana wa Tweets za Nikki Mbishi kwani mara kwa mara anazi-retweet na ku-ask watu wam-follow Nikki Mbishi (@NikkiZohan).

Monday, January 14, 2013

CHILLAH AKIRI KUVUTA BANGI PAMOJA NA KUTOA SABABU ZAKE


"MUZIKI WANGU KUKOSA SOKO NA UGUMU WA MAISHA VILINIFANYA NIVUTE BANGI" CHILLAH A.K.A CHICHI


Muimbaji wa Buttefly, Abubakar Katwila aka Q-Chilla amesema kuingia kwake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kulisababishwa na baadhi ya watu waliochangiakumrudisha chini kimuziki na kujikuta yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipiitia. 


Huku akikataa kuwataja kwa majina alisema watu hao walihakikisha kila anachokifanya hakifanikiwi na kujikuta katika wakati mgumu. Akiongea na Fina Mango kwenye kipindi cha Makutano cha Magic FM, Qchilla alisema alishindwa kujua amemkosea nani au nani amuombe msamaha. 

Hata hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia madawa hayo. Alipoulizwa anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye matumizi hayo alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na kuishika dini. 

Pia aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia aliingia katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela aliejaribu kumsaidia mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama aliyemsaidia marehemu Whitney Houston na kusisitiza wasanii wote ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya kujitokeza ili wasaidiwe na jamii.

Alisema kwa sasa anafanya muziki akilenga soko la kimatafifa zaidi akiwatolea mfano P-Square na kusema tatizo la wanamuziki wengi kuishia kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani pekee.

Chilla ambaye kwa sasa anajiita Chichi alimalizia kwa kusema kuwa hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa nyimbo kali.

HIKI NDIO KILICHOMKUTA WABABA KWA SASA


MSANII WA BSS 2012 (WABABA) AKABILIWA NA KESI YA KUTEMBEA NA MWANAFUNZI WA "FORM THREE" NA KUMTIA MIMBA


 Mapenzi yao yalianza tangu binti akiwa kidaato cha tatu lakini halikuwa penzi lenye mashamu shamu kwa kuwa wabababa alikuwa bado hajamiliki pesa na heshima katika jamii inayomzunguka kama sasa mara tuu baada ya kuchukua kifuta jasho cha bss na vijihela alivyopewa na mapapaa waliokubali kazi aliioifanya bss hivyo kuwa na kiburi kilichomfanya amtie mimba mwananfunz ambae aligundulika kuwa ametoa mimba mara taarifa za mahusiano ya wababa na mwanafunzi huyo kufikishwa kwa mama mzazi wa binti huyo. 

 
Wababa aliwekwa ndani kwa muda wa siku mbili na kesi bado ipo mahakamani na wazazi wa binti wameapa kumweka ndani wababa na kumfanya kama Babu Sea huku binti akiwa hajaonekana siku ya 4 sasa na kutokujulikana alipo kwa madai anampenda wababa na wakimfunga tu nae anakunywa sumu.