Tuesday, January 29, 2013

YAWEZEKANA A-Y AKAWA NDIO MSANII PEKEE TAJIRI KWA TANZANIA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na na mwenye tuzo kibao za kimataifa Ambwene Yesaya AY ni kati ya wasanii wanaomiliki pesa nyingi sana na mali kibao lakini hawapendi kujionyesha imefahamika. 

Chanzo makini na cha karibu na msanii huyo kimesema kuwa AY ni msanii anayemiliki pesa nyingi sana na ni kati ya wasanii wenye biashara nyingi sana ndani na nje ya nchi.


Chanzo hicho kiliendelea kupasha kuwa msanii huyo kwa sasa anamiliki mijengo kadhaa ndani ya bongo na maduka lukuki hasa ya nguo na Pub kadhaa japo msanii huyo hapendi kujulikana kama ni vyake kilisema chanzo hicho. 

AY anamiliki vitu vingi sana sema jamaa si mtu wakujionyesha lakini nataka ujue kuwa kuna uwezekano mkubwa jamaa akawa ndio mwanamuziki tajiri Tanzania kilisema chanzo hicho na kuendelea kumwaga za ndani kuwa juzi juzi AY alinunua nyumba hapa dar na yupo mbioni kuivunja na kujenga ghorofa.


Jamaa alizidi kutiririka na kuweka wazi kuwa kwa sasa AY anamiliki mjengo wa ki- star nchini kenya na ana maduka kadhaa katika nchi hiyo. 

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa AY mwenyewe aliwahi kukaririwa akisema kuwa ni kweli ana mpango wa kununua nyumba kenya na kufungua maduka kadhaa hivyo ameona bora kununua nyumba nchini humo kwakuwa ni sehemu ambayo anaenda sana kwa shughuli zake na apate pakufikia na kupanga mambo yake badala ya kukaa hotelini. 

Mwamuziki huyo licha ya kumiliki vyote hivyo bado ana miliki kampuni yake ya Unity Entertainment ambayo inaendelea kukua siku hadi siku na sasa ikiwa na wasanii kama Ommy Dimpoz, Feza Kessy na Stereo kwenye roaster yake.

AY ni msanii wa kwanza Tanzani kwa upande wa muziki mwenye connection kubwa na wasanii marufu wa afrika na ulaya, kwa Afrika alionao karibu kwa ajili ya kazi ni pamoja na P Square, Jay martins, Jose chamilione, Bebe Cool, Prezzo, Aman, Alpha Kwa upande wa marekani ni Romeo,D'Banji,Akon,Master P, Sean King Stone.

No comments:

Post a Comment