Monday, January 14, 2013

POLENI IFM KWA MAJANGA YALIOWAKUMBA

UBAKAJI NA ULAWITI WAWAFANYA WANAFUNZI WA IFM WAANDAMANE

Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wameandamana leo majira ya adhuhuri hadi kwenye  Wizara ya Mambo ya Ndani wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara.

Wanafunzi hao walidai kuwam, siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu ni kuwa, siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndiyo siku wenzao wawili wakiume walipovamiwa na kulawitiwa.

Majambazi hao wamekua wakidai wapewe laptops, simu na fedha na kama mwanafunzi anakataa, humlawiti.

Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM alizungumza leo na Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo alisema, "Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo…" ndipo kamanda Kova aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane naye waende hadi Kigamboni kwenye Kituo waliporipoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.

------------------------------------------------------------------

No comments:

Post a Comment