Tuesday, January 15, 2013
BEN POL AMETOFAUTIANA SANA NA STAMINA
Msanii wa RnB ambaye kwa sasa anatamba na Track yake ya Pete, Ben Polameamua kufunguka kuhusiana na kuvuja au ku-leak kwa nyimbo (Nyimbo zao kusikika kabla wao hawajazitoa). Mtazamo wa Ben Pol unatofautiana sana naStamina.
Ben Pol amezungumzia swala la ku-leak kwa nyimbo za wasanii sambamba na kufunguka kuhusu moja ya nyimbo zake ku-leak na hatua aliyochukua. Ben Polalisema:
"Nyimbo yangu iki-leak ikapendwa naona sio tatizo... Maneno ili-leak lakini ndo imekuwa wimbo wa watu, na imenipa shows na Heshima... Saa zingine tunatumia nguvu nyingi na muda, pia gharama bure ku-promote nyimbo ambazo watu wameshazikataa tangia siku nyimbo hizo zinapotoka..."
- Ben Pol.
Stamina alighairi kutoa track yake ya 'Ushauri Nasaha' baada ya ku-leak na badala yake akatoa track yake ya 'Wazo la Leo'. Kuvuja kwa Track ya 'Ushauri Nasaha' kulimuumiza sana Stamina lakini baada ya kutiwa moyo na kupewa ushauri na Fid Q, Stamina ali-record 'Wazo la Leo' kwa P-Funk Majani ambapo mpaka sasa ngoma hiyo inafanya vizuri kupita kiasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment