Friday, January 4, 2013
PICHA MBALIMBALI ZA NYUMBANI KWA SAJUKI AMBAKO MSIBA ULIPOFANYIKA
Mazishi ya msanii mahiri wa tasnia ya filamu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia juzi yanatarajiwa kufanyika leo mchana katika makaburi ya Kisutu baada ya sala ya Ijumaa. Akiongea na mwenyekiti wa kamati ya mazishi Steve Nyerere amesema kuwa msiba huu unasimamiwa na shirikisho na wasanii wa filamu na wadau wa tasnia hiyo.
“Ratiba ya mazishi leo saa tatu asubuhi mwili wa marehemu utaletwa hapa nyumbani kwa marehemu Tabata utaswaliwa na baada ya hapo tutaelekea na mwili wa marehemu Msikiti wa Upanga tukitoka Upanga tutaelekea Kisutu kwajili ya mazishi na baada ya mazishi tutarudi hapa nyumbani kwakuwa kutakuwa kuna mambo ambayo yatakuwa yanaendelea,” amesema Steve.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment