Friday, January 4, 2013

BONGE LA PARTY KWA KUTOKA LULU BAADA YA KUWA URAIANI



Elizabeth Michael ‘Lulu’.
 STAA wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye kwa hivi sasa yuko nyuma ya nondo kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba ameandaliwa bonge la pati atakapotia maguu uraiani. 
Akichonga  juzikati, mmoja wa wasanii wenzake, Sabrina Rupia ‘Cath’ alisema kuwa, wanaomba usiku na mchana ili mwenzao huyo apewe dhamana na arudi uraiani na hiyo siku kwa furaha watamuandalia bonge la pati.
“Kwa kweli Mungu amsaidie apewe hiyo dhamana, siku atakaporudi uswahilini tumepanga kumdondoshea bonge la pati,” alisema Cath.
Hivi karibuni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar, ilihamishia kesi ya Lulu Mahakama Kuu baada ya mwendesha mashitaka wa serikali kubadili mashitaka ya kuua na kuwa ya kuua bila ya kukusudia hivyo kutoa mwanga wa kuwepo kwa dhamana.

No comments:

Post a Comment