Friday, January 4, 2013

WASIA WA MWISHO WA SAJUKI


Mwigizaji Dinno alikua rafiki mkubwa sana wa Marehemu Sajuki na ndio alikua analala hospitali na Sajuki pale Muhimbili.

Ameongea  AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kutoa maneno ya mwisho ambayo aliyasikia kutoka kwa Sajuki akimzungumzia mke wake ambae ni Wastara.

Kwa haraka haraka mwigizaji Wastara amesifiwa sana na watu mbalimbali kwa moyo wake wa ushujaa wa ukweli wa upendo kwa Sajuki japo walipitia matatizo makubwa na mengi kwenye maisha yao.

Masanja Mkandamizaji na Arnold Kayanda ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania waliopaza sauti zao kupitia mitandao ya kijamii kumsifia Wastara kwa moyo wa upendo.

Tukirudi kwa Dinno, namkariri akisema “tulipokuwa Arusha sisi watatu tu Sajuki alionyesha ishara ya kukata tamaa, siku moja tulikua hotelini usiku kama saa tisa hivi Wastara alikuja kuniamsha kwenye chumba changu nikaenda kwa Sajuki, alikua anaumwa sana akamwambia Wastara naomba mpigie mama niongee nae, Sajuki akamwambia mama yake mzazi kwamba Wastara nampenda sana, kanizalia mtoto mzuri anaitwa Farhini, naomba msimsumbue naomba msimpe shida yoyote amenisaidia sana, naomba mumwachie Farhini amlee amtunze mtamuona, yalikua maneno mazito sana mpaka machozi yakawa yananitoka”

Mbali  na hayo, Dinno amesema jambo jingine ambalo Sajuki aliliongea mwishoni ni kuhusu upendo miongoni mwa wasanii wa movie Tanzania, namkariri akisema “alikua ananiambia hebu jitahidi kuwa unakaa na wasanii, unajua sisi hatupendani Dinno ila mimi iko siku nitakuja kuropoka nikae na watu niwazungumzie tuweke upendo pamoja, tukishapendana tutafanya kitu Dinno”
Source: vituko vya mtaa@blog

No comments:

Post a Comment