Saturday, January 19, 2013

SHAKIRA NA PIQUE NI WAZAZI WATARAJIWA



Ready and waiting: Shakira and Gerard Piqué have posed for a series of intimate shots, showing off her baby bump  

Shakira na mpenzi wake mcheza mpira  Gerard Piqué  wameachia picha kadhaa zinazoonyesha uka uzito wake wakisherehekea ujio wa mtoto wao wakwanza
 akiwa amevaa bikini top na sketi, huku boyfriend akiwa hana shati, picha inaonyesha ukaribu wao wakiwa wanasuburi ujio wa mtoto wao wakwanza wakiume

 Picha hizi ambazo zilipigwa na Jaume Laiguana, zilitupiwa kwenye mtandao mara baada ya wawili hao kuamua kuungana na UNICEF ku host a virtual baby shower.

Not long now: The Colombian singer shows off her amazing pregnant shape in the snaps wearing just a pair of loose-fitting trousers and a bikini top  

Shakira, 35, amefata nyayo za ma staa kama  Demi Moore and Britney Spears,  ambao walishawahi kupiga picha za namna hii wakati wa muda wa mwisho mwisho wa mimba zao.

Pregnant and proud: Shakira and her footballer beau Gerad Pique have posed for this beautiful picture which shows the singer in all her pregnant glory 

Shakira na mchezaji huyu wa FC Barcelona walikutana mwaka 2010, pale alipotokea kwenye music video ya Shakira, (waka waka, this time for Africa) ambao ulikua ndio wimbo wa kombe la dunia.
Beautiful: In the second image, taken as part of the 35-year-old's virtual baby shower alongside UNICEF, Sharkira stands in a flowing almond gown

JOH MAKINI ATOKA KI UTU UZIMA


JOH MAKINI: MASHABIKI WANGU HUU NDIYO UJI WANGU MPYA SOON KUTOKA

Msanii rapper kutoka Arusha, maarufu kama Joh Makini Mwamba wa kaskazini baada ya kufanya vizuri mwaka jana katika tasnia hii ya muziki wa Bongo Fleva,mwaka huu amejipanga vema na siku za hivi karibuni anatarajia kuachia video yake mpya inayokwenda kwa jina la KI-UTU-UZIMA.Kaa tayari kwa uji huo mpya kutoka kwa Joh Makini

ALINGO - P SQUARE (VIDEO)


LISTEN - BELLE 9 (VIDEO)


Tuesday, January 15, 2013

NIKKI MBISHI NA KINGZILLA KUFANYA MIXTAPE YAO





Wakali wa Hiphop Music BongoNikki Mbishi na Godzilla ambao wote walipata nafasi ya kusikika baada ya mashindano ya Freestyle ambayo yalikua yakiendeshwa na Clouds fm wameamua kufanya Project ya pamoja.

Nikki Mbishi ambaye alitamba na track ya Playboy ambayo alimshirikisha Ben Pol, jana kwenye ukurasa wake wa Facebook ali-announce mpango wa kufanya Project hii na GodzillaNikki aliandika:

"Nikki Mbishi na Godzilla kazini, jiandae kwa Mixtape yetu ya pamoja iitwayo 'KKK'..."

Lately kwenye mtandao wa TwitterGodzilla amekua supporter mkubwa sana wa Tweets za Nikki Mbishi kwani mara kwa mara anazi-retweet na ku-ask watu wam-follow Nikki Mbishi (@NikkiZohan).

BEN POL AMETOFAUTIANA SANA NA STAMINA



Msanii wa RnB ambaye kwa sasa anatamba na Track yake ya PeteBen Polameamua kufunguka kuhusiana na kuvuja au ku-leak kwa nyimbo (Nyimbo zao kusikika kabla wao hawajazitoa). Mtazamo wa Ben Pol unatofautiana sana naStamina

Ben Pol amezungumzia swala la ku-leak kwa nyimbo za wasanii sambamba na kufunguka kuhusu moja ya nyimbo zake ku-leak na hatua aliyochukua. Ben Polalisema:


"Nyimbo yangu iki-leak ikapendwa naona sio tatizo... Maneno ili-leak lakini ndo imekuwa wimbo wa watu, na imenipa shows na Heshima... Saa zingine tunatumia nguvu nyingi na muda, pia gharama bure ku-promote nyimbo ambazo watu wameshazikataa tangia siku nyimbo hizo zinapotoka..."
Ben Pol.

Stamina alighairi kutoa track yake ya 'Ushauri Nasaha' baada ya ku-leak na badala yake akatoa track yake ya 'Wazo la Leo'. Kuvuja kwa Track ya  'Ushauri Nasaha'  kulimuumiza sana Stamina lakini baada ya kutiwa moyo na kupewa ushauri na Fid QStamina ali-record  'Wazo la Leo'  kwa P-Funk Majani ambapo mpaka sasa ngoma hiyo inafanya vizuri kupita kiasi.

Monday, January 14, 2013

CHILLAH AKIRI KUVUTA BANGI PAMOJA NA KUTOA SABABU ZAKE


"MUZIKI WANGU KUKOSA SOKO NA UGUMU WA MAISHA VILINIFANYA NIVUTE BANGI" CHILLAH A.K.A CHICHI


Muimbaji wa Buttefly, Abubakar Katwila aka Q-Chilla amesema kuingia kwake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kulisababishwa na baadhi ya watu waliochangiakumrudisha chini kimuziki na kujikuta yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipiitia. 


Huku akikataa kuwataja kwa majina alisema watu hao walihakikisha kila anachokifanya hakifanikiwi na kujikuta katika wakati mgumu. Akiongea na Fina Mango kwenye kipindi cha Makutano cha Magic FM, Qchilla alisema alishindwa kujua amemkosea nani au nani amuombe msamaha. 

Hata hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia madawa hayo. Alipoulizwa anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye matumizi hayo alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na kuishika dini. 

Pia aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia aliingia katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela aliejaribu kumsaidia mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama aliyemsaidia marehemu Whitney Houston na kusisitiza wasanii wote ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya kujitokeza ili wasaidiwe na jamii.

Alisema kwa sasa anafanya muziki akilenga soko la kimatafifa zaidi akiwatolea mfano P-Square na kusema tatizo la wanamuziki wengi kuishia kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani pekee.

Chilla ambaye kwa sasa anajiita Chichi alimalizia kwa kusema kuwa hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa nyimbo kali.

POLENI IFM KWA MAJANGA YALIOWAKUMBA


UBAKAJI NA ULAWITI WAWAFANYA WANAFUNZI WA IFM WAANDAMANE


Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wameandamana leo majira ya adhuhuri hadi kwenye  Wizara ya Mambo ya Ndani wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara.

Wanafunzi hao walidai kuwam, siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu ni kuwa, siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndiyo siku wenzao wawili wakiume walipovamiwa na kulawitiwa.

Majambazi hao wamekua wakidai wapewe laptops, simu na fedha na kama mwanafunzi anakataa, humlawiti.

Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM alizungumza leo na Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo alisema, "Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo…" ndipo kamanda Kova aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane naye waende hadi Kigamboni kwenye Kituo waliporipoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.

------------------------------------------------------------------





UBAKAJI NA ULAWITI WAWAFANYA WANAFUNZI WA IFM WAANDAMANE


Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wameandamana leo majira ya adhuhuri hadi kwenye  Wizara ya Mambo ya Ndani wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara.

Wanafunzi hao walidai kuwam, siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu ni kuwa, siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndiyo siku wenzao wawili wakiume walipovamiwa na kulawitiwa.

Majambazi hao wamekua wakidai wapewe laptops, simu na fedha na kama mwanafunzi anakataa, humlawiti.

Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM alizungumza leo na Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo alisema, "Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo…" ndipo kamanda Kova aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane naye waende hadi Kigamboni kwenye Kituo waliporipoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.

------------------------------------------------------------------




HIKI NDIO KILICHOMKUTA WABABA KWA SASA


MSANII WA BSS 2012 (WABABA) AKABILIWA NA KESI YA KUTEMBEA NA MWANAFUNZI WA "FORM THREE" NA KUMTIA MIMBA


 Mapenzi yao yalianza tangu binti akiwa kidaato cha tatu lakini halikuwa penzi lenye mashamu shamu kwa kuwa wabababa alikuwa bado hajamiliki pesa na heshima katika jamii inayomzunguka kama sasa mara tuu baada ya kuchukua kifuta jasho cha bss na vijihela alivyopewa na mapapaa waliokubali kazi aliioifanya bss hivyo kuwa na kiburi kilichomfanya amtie mimba mwananfunz ambae aligundulika kuwa ametoa mimba mara taarifa za mahusiano ya wababa na mwanafunzi huyo kufikishwa kwa mama mzazi wa binti huyo. 

 
Wababa aliwekwa ndani kwa muda wa siku mbili na kesi bado ipo mahakamani na wazazi wa binti wameapa kumweka ndani wababa na kumfanya kama Babu Sea huku binti akiwa hajaonekana siku ya 4 sasa na kutokujulikana alipo kwa madai anampenda wababa na wakimfunga tu nae anakunywa sumu.

Thursday, January 10, 2013

JAY DEE AENDELEA VIZURI NA SAFARI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO




Maendeleo ya safari yao:
January 8 – Mandara Hut(2700m) – Horombo Hut(3720m)
Masaa ya kutembea: 5
January 9: Acclimatization Day at Horombo Hut
Masaa ya kutembea: 4
January 10: Horombo Hut(3720m) – Kibo Hut(4703m)
Masaa ya kutembea: 5
Baadaye leo waanza safari ya kuelekea Uhuru Peak(5895m) kupitia Gillman’s point(5685m)


Hali zao kiafya
Gadner, Lady Jaydee na mpiga picha wao Justin wako fit na wana uwezo wa kuendelea hadi kituo kinachofuata.

WAZEE WA POWER WINDOW WAMLIZA TENA MH.TEMBA




Ikiwa imepita miezi miwili tu tangu wezi waifanyie kitu mbaya gari ya Mheshimiwa Temba aina ya Verossa, kwa mara nyingine tena wezi wameiba vifaa vya gari lake.
Taarifa hiyo imetolewa na leo na Chege kupitia Twitter ambaye ameandika:

Wazee wa power window mtuhurumie!watu hata bila huruma wamemuibia tena vitu vya gari temba,lkn mwisho wa mchezo huu hautokua mzuri ni lawama.

Mwishoni mwa mwaka uliopita watu wasiojulikana waliiba vifaa vya gari lake wakati lilipokuwa limeegeshwa nyumbani kwake.

Vifaa vilivyoibiwa katika tukio la kwanza ni pamoja na power window, side mirror zote taa za nyuma, radio leseni hadi madaftari yake ya shule....

Saturday, January 5, 2013

WEMA KUWA PRESENTER NDANI YA CHOICE FM


WEMA SEPETU APEWA SHAVU LA KUENDESHA TOP 20 YA CHOICE FM


WEMA  SEPETU  siku ya Leo mchana anatakuwa live akitangaza.... 

Hii itakuwa ni Mara Ya kwanza kwa Wema sepetu kuwasha kipaza sauti na kuendesha show Ya redio kwa masaa mawili...

 Maybe hii itakuwa ni mwanzo wa sauti yake kusikika redioni.... Hebu tune to Choice Fm today 102.6 Fm ili toe  kama  Anaiweza hii kazi 

Ulipata kuisikia ngoma hii....???

Machalii flani wa arusha wakipiga remix ya ule wimbo wa kigoma na kubatiza jina la kiroba..


Download hapa

Friday, January 4, 2013

DEAR GOD - KALA JEREMIAH (MP3)

Download hapa

NIMERUDI - CHIDI BENZ FEAT DULLY SYKES (MP3)

Download hapa

NIPENDE - MR. BLUE FEAT WALTER (MP3)

Download hapa

UKIONA DALILI HIZI ELEWA UNASALITIWA


 Hiki ni kipindi kibaya sana katika mapenzi na mtu anapotokewa na jambo kama hili huathirika sana kisaikolojia kiasi cha kuwa tayari kufanya kitu chochote ili kulipa kisasi. Sio ajabu kusikia mtu fulani kamchinja mkewe, kamuua mumewe, kapigana vikali, kafanya madhara makubwa au kajinyonga baada ya kugundua kuwa mwenzi wake anamsaliti
Kwa kutambua hilo, ndiyo maana nimekuandalia dondoo muhimu ambazo zitakufanya umgundue mapema mpenzi ‘anayekuzunguka’ ili uamue nini cha kufanya kabla mambo hayajazidi kuharibika.
DALILI ZA MTU ANAYEKUSALITI
Kuna dalili nyingi ambazo mtu anayefanya usaliti nje ya uhusiano wake, huzionesha. Kuwa makini kwani sio kila uonapo dalili moja au mbili kati ya hizi, inamaanisha mwenzi wako anakusaliti.
Unapaswa kuchunguza dalili nyingi kwa pamoja ndipo uwe na uhakika kuwa unasalitiwa.
*Kusingizia kazi hata muda wa ziada
Mtu anayekusaliti huanza kuwa na visingio vingi vya kuchelewa kurudi nyumbani. Kila mara atakwambia kuwa alikuwa na kazi za ziada (overtime) na ndio zimemfanya achelewe kurudi nyumbani(Kwa wale ambao ni wafanyakazi). Mara nyingi huu huwa ni uongo kwani uwezekano mkubwa ni kuwa ametoka kukutana na mpenzi wa nje na kazi huwa ni kisingizio anachotumia kuficha uchafu aliokuwa anaufanya.
Inawezekana kabisa mtu akatafuta ushahidi hata wa marafiki zake anaofanya nao kazi kuthibitisha kuwa ni kweli alikuwa kazini wakati si kweli. Kuwa makini sana na watu wa aina hii.
*Kuwahi sana kuondoka anapokwenda kazini asubuhi
Mbinu hii hutumika sana na mtu ambaye ameanzisha uhusiano na kuisaliti ndoa yake na mtu wanayefanya naye kazi katika ofisi moja.
Asubuhi hupenda kuwahi kazini kuliko kawaida ili akifika apate muda wa kuwa na mpenzi wake hata kwa muda mfupi kabla wafanyakazi wengine hawajafika.
Wanaweza pia kuutumia muda huu kwenda sehemu ya faragha na hata kuvunja amri ya sita.
* Kunukia pombe au pafyumu ngeni
Wakati mwingine, mwenza anayekusaliti anaweza akakudanganya kuwa anatoka kazini lakini wakati huohuo akawa ananuka pombe au harufu ya pafyumu ngeni.
Dalili hii huchukuliwa kuwa muhimu sana kwani endapo mwenzi wako ataonesha dalili hii, ni dhahiri kuwa muda mfupi uliopita alikuwa akirusha roho na mtu mwingine. Ni wajibu wa kila mmoja kuwa makini sana na mwenza wake kwani dalili hii inapoonekana, huwa ni hatari sana.
* Kuwa bize na simu muda mwingi
Endapo hukuzoea kumuona mwenzi wako akiwa bize na simu kwa muda mrefu, halafu ikatokea anaanza kuonesha mabadiliko ya haraka, akiutumia muda mwingi kusoma na kuandika sms kwenye simu yake, basi kuna uwezekano mkubwa akawa ameanza kukusaliti.
Inawezekana pia kuwa anapokuwa mbali na wewe, unapompigia simu yake inakuwa bize muda mwingi, huku akiwa hakwambii moja kwa moja huwa anazungumza na nani. Hata anapozungumza na wewe, akili yake huwa iko mbali.
* Kukosa utulivu anapokuwa na wewe
Mwenzi ambaye ameanza kukusaliti, huwa na kawaida ya kukosa kabisa utulivu anapokuwa na wewe. Kama mpo naye ndani basi utaona akijikanyaga mara kwa mara, akidondosha vitu na kuwa na papara zisizoelezeka.
Hii hutokea kwa sababu nafsini mwake huwa anahukumiwa kwa kitendo anachokufanyia, hivyo hujaribu kuzificha hisia zake za ndani, lakini badala ya kuzificha ndiyo huzidi kuzionesha. Pia huwa ni kwa sababu anapokuwa na wewe, akili yake huwa inamuwaza mtu mwingine tofauti kwa hiyo anakuwepo kimwili lakini kiakili anakuwa mbali sana, hivyo umakini hupungua sana.
*Kuondoka nyumbani kwa kuzira mnapogombana
Wenzi wengi hulalamika kuwa wenzi wao wanapoanza kuonesha mabadiliko ya kitabia, inapotokea wakakwazana wakiwa ndani ya nyumba hata kwa jambo ambalo ni dogo, mmoja hujifanya kukasirika sana na kuondoka nyumbani bila kueleza anapokwenda, na anaporudi huwa amebadilika kabisa.
Uwezekano mkubwa ni kwamba mnapogombana, mwenzi wako anaweza kuwa anaitumia nafasi hiyo kikamilifu kwa kukutana na mpenzi wa nje kwa lengo la kujiliwaza.
*Kuanza kupendeza sana kimavazi anapotaka kutoka
Inaelezwa kuwa unapoona mwenzi wako akibadilika ghafla kitabia na kupenda kujiremba sana, kujipodoa na kuvaa nguo zinazomzidishia mvuto kuliko kawaida anapokuwa anataka kutoka, yawezekana anayafanya yote hayo kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wake mpya.
Unapaswa kuwa makini sana unapoona mabadiliko kama haya. Pia utamuona akianza kubadili aina ya mavazi aliyokuwa akipendelea kuyavaa, na zaidi atakuwa akipendelea mavazi yanayomfanya aonekane kijana.
*Kubadili marafiki ghafla
Unapogundua kuwa mwenzi wako amebadilisha marafiki na kuanza kushirikiana na watu wanaotia hofu, basi elewa kuna jambo nyuma ya pazia.
Unaweza kuona mwenzi wako akianza kuwa na uhusiano wa karibu na watu waliomzidi sana umri au ambao ni wadogo sana kuliko yeye.
Urafiki wa aina hii huwa ni kwa sababu kuna siri wanazofichiana au kuna mambo wanayoyafahamu wenyewe na hawapendi mtu mwingine afahamu.
*Kushindwa kupokea simu anapokuwa na wewe
Wengi wamekuwa wakilalamikia sana tabia hii, ambapo wenzi wao hushindwa kupokea simu wanapokuwa nao. Unakuta simu inaita halafu mwenzio anainuka na kwenda kupokelea nje

WASIA WA MWISHO WA SAJUKI


Mwigizaji Dinno alikua rafiki mkubwa sana wa Marehemu Sajuki na ndio alikua analala hospitali na Sajuki pale Muhimbili.

Ameongea  AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kutoa maneno ya mwisho ambayo aliyasikia kutoka kwa Sajuki akimzungumzia mke wake ambae ni Wastara.

Kwa haraka haraka mwigizaji Wastara amesifiwa sana na watu mbalimbali kwa moyo wake wa ushujaa wa ukweli wa upendo kwa Sajuki japo walipitia matatizo makubwa na mengi kwenye maisha yao.

Masanja Mkandamizaji na Arnold Kayanda ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania waliopaza sauti zao kupitia mitandao ya kijamii kumsifia Wastara kwa moyo wa upendo.

Tukirudi kwa Dinno, namkariri akisema “tulipokuwa Arusha sisi watatu tu Sajuki alionyesha ishara ya kukata tamaa, siku moja tulikua hotelini usiku kama saa tisa hivi Wastara alikuja kuniamsha kwenye chumba changu nikaenda kwa Sajuki, alikua anaumwa sana akamwambia Wastara naomba mpigie mama niongee nae, Sajuki akamwambia mama yake mzazi kwamba Wastara nampenda sana, kanizalia mtoto mzuri anaitwa Farhini, naomba msimsumbue naomba msimpe shida yoyote amenisaidia sana, naomba mumwachie Farhini amlee amtunze mtamuona, yalikua maneno mazito sana mpaka machozi yakawa yananitoka”

Mbali  na hayo, Dinno amesema jambo jingine ambalo Sajuki aliliongea mwishoni ni kuhusu upendo miongoni mwa wasanii wa movie Tanzania, namkariri akisema “alikua ananiambia hebu jitahidi kuwa unakaa na wasanii, unajua sisi hatupendani Dinno ila mimi iko siku nitakuja kuropoka nikae na watu niwazungumzie tuweke upendo pamoja, tukishapendana tutafanya kitu Dinno”
Source: vituko vya mtaa@blog

BONGE LA PARTY KWA KUTOKA LULU BAADA YA KUWA URAIANI



Elizabeth Michael ‘Lulu’.
 STAA wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye kwa hivi sasa yuko nyuma ya nondo kwa kosa la kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba ameandaliwa bonge la pati atakapotia maguu uraiani. 
Akichonga  juzikati, mmoja wa wasanii wenzake, Sabrina Rupia ‘Cath’ alisema kuwa, wanaomba usiku na mchana ili mwenzao huyo apewe dhamana na arudi uraiani na hiyo siku kwa furaha watamuandalia bonge la pati.
“Kwa kweli Mungu amsaidie apewe hiyo dhamana, siku atakaporudi uswahilini tumepanga kumdondoshea bonge la pati,” alisema Cath.
Hivi karibuni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar, ilihamishia kesi ya Lulu Mahakama Kuu baada ya mwendesha mashitaka wa serikali kubadili mashitaka ya kuua na kuwa ya kuua bila ya kukusudia hivyo kutoa mwanga wa kuwepo kwa dhamana.

PICHA MBALIMBALI ZA NYUMBANI KWA SAJUKI AMBAKO MSIBA ULIPOFANYIKA

Mazishi ya msanii mahiri wa tasnia ya filamu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia juzi yanatarajiwa kufanyika leo mchana katika makaburi ya Kisutu baada ya sala ya Ijumaa. Akiongea na mwenyekiti wa kamati ya mazishi Steve Nyerere amesema kuwa msiba huu unasimamiwa na shirikisho na wasanii wa filamu na wadau wa tasnia hiyo.
“Ratiba ya mazishi leo saa tatu asubuhi mwili wa marehemu utaletwa hapa nyumbani kwa marehemu Tabata utaswaliwa na baada ya hapo tutaelekea na mwili wa marehemu Msikiti wa Upanga tukitoka Upanga tutaelekea Kisutu kwajili ya mazishi na baada ya mazishi tutarudi hapa nyumbani kwakuwa kutakuwa kuna mambo ambayo yatakuwa yanaendelea,” amesema Steve.
Kamati ya mazishi ikiteta jambo na  Kiongozi wa shilikisho la filamu
Kamati ya mazishi ikiteta jambo na Kiongozi wa shilikisho la filamu
Stive Nyerere akipokea mchango wa mazishi kutoka chuo cha filamu cha Pastor Myamba
Stive Nyerere akipokea mchango wa mazishi kutoka chuo cha filamu cha Pastor Myamba
Wasanii wa filamu wakiwa wamekaa kimya wakisikiliza jambo kutoka kwa Uongozi wa shilikisho la Filamu
Wasanii wa filamu wakiwa wamekaa kimya wakisikiliza jambo kutoka kwa Uongozi wa shilikisho la Filamu
Kiongozi wa shilikisho la filamu akitoa mawili matatu kwa wasanii wa filamu
Kiongozi wa shilikisho la filamu akitoa mawili matatu kwa wasanii wa filamu
Mdau akitoa mchango wa mazishi
Mdau akitoa mchango wa mazishi
Mdau akitoa mchango wa mazishi
Mdau akitoa mchango wa mazishi
Masanja Mkandamizaji
Masanja Mkandamizaji
Waigizaji wakiwa na uzuni

Viongozi wa kamati ya mazishi wakijaliana jambo na wadau wa filamu
Viongozi wa kamati ya mazishi wakijadiliana jambo na wadau wa filamu
Mdau wa filamu akitoa pole na kuwafariji ndugu wa marehemu
Mdau wa filamu akitoa pole na kuwafariji ndugu wa marehemu
Waigizaji wa filamu wakiwa wamekaa kwa uzuni
Waigizaji wa filamu wakiwa wamekaa kwa huzuni
wasanii wa filamu
wasanii wafilamu
Baadhi ya wasanii wakiwa katika pozi la uzuni
Baadhi ya wasanii wakiwa katika pozi la uzuni
Mwigizaji katika pozi
Mwigizaji katika pozi
Waigizaji wa filamu
Waigizaji wa filamu
Steve na Monalisa
Stive na Monalisa
Source:viyuko vya mtaa@blog